pmbet

Marubani wa Tanzania wakodiwa kufundisha Nigeria

Eric Buyanza

May 6, 2024
Share :

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeingia makubaliano ya kupeleka marubani wake kufundisha na kusimamia ndege mpya za Airbus A220 za Kampuni ya Ndege ya Ibom iliyopo nchini Nigeria. 

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema kuwa kampuni yake imetoa marubani wake waandamizi wawili. 

Marubani hao wa ATCL watakuwa na jukumu la kufundisha na kusimamia mafunzo kwa vitendo hadi pale watakapojiridhisha kuwa marubani wanafunzi na walimu wao wamefikia viwango vinavyotakiwa vya kuendesha ndege hizo, alisema Matindi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet