Marudio ya uchaguzi serikali za mitaa kata ya Kinyala.
Joyce Shedrack
December 4, 2024
Share :
Uchaguzi wa Marudio katika kitongoji cha Ipuga kijiji cha Lukata kata ya kinyala umeanza Asubuhi hii baada ya wagombea wawili kufungana katika matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27.11.2024
Vyama viwili vya siasa ( CCM & CHADEMA) Vinawania kiti hiki muhimu kwa utawala bora katika Serikali za Mitaa.
Katika Hali ya Kufurahisha kiti hiki kinawaniwa na Wanawake pekee na hakuna kijiji wa kitongoji katika wilaya ya Rungwe kilichokuwa kinagombaniwa na wanawake pekee bali na Kitongoji cha Ipugi tu
Katika Picha Wananchi Wawili Wanaoonekana kwa Mbele ndiyo wagombea wa nafasi hii.
Uchaguzi unatarajiwa kuhitimishwa saa 4:30 Alasiri ambapo mshindi anatarajiwa kupatikana.