pmbet

Marufuku kuingia na chupa viwanjani kwenye Kombe la Dunia

Eric Buyanza

June 4, 2026
Share :

Fifa imefanya uamuzi wa dakika za mwisho kupiga marufuku mashabiki, kubeba chupa za maji zinazoweza kutumika tena viwanjani kwenye Kombe la Dunia.

Fifa imesema uamuzi huo umefanywa ili "kuzuia hatari na majeraha kwa wachezaji na wahudhuriaji", na vitu vingine kama vile makopo na vikombe pia vimepigwa marufuku.

 

Fainali hizo zinazofanyika katika nchi za Canada, Marekani na Mexico, mechi zake zitakuwa kwenye joto kali, na ili kutoa angalizo chupa za maji hazitotakiwa uwanjani kwa mashabiki.

Aidha fifa imesema kutakuwa na mifumo ya kupoza hewa na maji ya kunywa yatauzwa ndani ya uwanja kwa mashabiki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet