Masaka Kids wa Uganda wafanya show Barca ikiiua Valencia
Sisti Herman
April 30, 2024
Share :
Kundi la watoto wanaolelewa kwenye kituo cha yatima kutoka Uganda maarufu mitandaoni Masaka kids, usiku wa jana walipata bahati ya kipekee kutumbuiza kwenye mechi ya ligi kuu ya soka Uhispania, Barcelona dhidi ya Valencia, iliyochezwa Uwanjani Montjuic.
Kwenye mchezo huo ambao Barca walibuka na ushindi wa 4-2, watoto hao walisherehesha wakati wa mapumziko.