Mashabiki elfu kumi kuingia kwa Mkapa leo.
Joyce Shedrack
August 6, 2025
Share :
Shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kuwa mashabiki 10000 wa kwanza wa jukwaa la Mzunguko watakaofika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa watapata nafasi ya kuingia bure kutazama mchezo wa Taifa Stars na Mauritania.
“Wanetu wa Mzunguko watu 10,000 wa kwanza mnapata ofa ya tiketi ya kuingia uwanjani bila kulipa, unachotakiwa kufanya beba Kadi yako ya N Card suala la tiketi ya kuingia tuachie sisi, utaangalia mechi zote mbili”
Mchezo wa kwanza wa kundi B utapigwa kuanzia saa 11:00 Jioni ukizihusisha timu za Taifa za Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Mauritania ukitarajiwa kuanza saa 2:00 usiku.