"Mashabiki hawatanishawishi kubakia Bayern Munich" - Thomas Tuchel
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel anasema hatakubali "kushawishiwa" na ombi la kumtaka abakie katika klabu hiyo.
Ombi la kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 kusalia Allianz Arena limetiwa saini na zaidi ya mashabiki 12,000.
Bayern ilitangaza mwezi Februari kwamba Tuchel ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.