Mashabiki wa Arsenal watinga kanisani kutoa shukrani baada ya ushindi
Eric Buyanza
January 22, 2024
Share :
Mashabiki wa Arsenal wa jijini Nairobi nchini Kenya, wamekusanyika kanisani Jumapili ya jana wakifanya maombi na kutoa shukrani kwa Mungu baada ya timu yao kuwalaza Crystal Palace 5-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi.
Wakiwa wamevalia tisheti zao za Gunners, mashabiki hao waliimba kwa furaha huku wakicheza wakati wa ibada ya asubuhi.
Pia walitoa maombi wakitumaini kuendelea kupata mafanikio kwa Arsenal katika msimu unaoendelea.
Arsenal kwa sasa wanalingana pointi na Manchester City, ambao wana mchezo mkononi dhidi ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London, na pointi tano nyuma ya Liverpool walio kileleni mwa jedwali.