Mashabiki wa Trump wavaa bendeji feki kumuunga mkono
Eric Buyanza
July 20, 2024
Share :
Katika hali ya kushangaza wafuasi wa Chama cha Republican wameonekana wakiwa wamevaa bendeji feki masikioni kama aliyokuwa amevalishwa Trump baada ya kujeruhiwa na risasi kwenye sikio lake.
Wanachama hao wanasema wameamua kuvaa hivyo kama njia ya kumuunga mkono Trump kwenye mbio zake za kugombea Urais wa Marekani ikiwa ni siku chache baada ya kunusurika kuuawa.