pmbet

Mashabiki wafariki wakishangilia timu yao Afcon

Sisti Herman

January 23, 2024
Share :

Mashabiki sita [6] nchini Guinea wamefariki wakati wakishangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Gambia kwenye fainali za mataifa ya Afrika [1-0].

 

Mashabiki waliingia kushangilia barabarani katika mji mkuu wa Guinea Conakry wakiwa na magari pamoja na pikipiki, lakini aina hii ya ushangiliaji ilipelekea ajali hiyo mbaya.

 

Watu watatu wamefariki baada ya pikipiki mbili kugongana zikiwa kwenye mwendo mkali, na watu wengine kadhaa kujeruhiwa.

 

Aguibou Camara aliipatia goli timu yake ya Guinea baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Morgan Guilavogui na kuihakikishia kuvuna alama tatu mhimu timu hiyo. Ni ushindi ambao uliipandisha timu hiyo hadi nafasi ya pili ya msimamo wa kundi C.

 

Guinea ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora wanapaswa kushinda au kutoa sare kwenye mchezo wao dhidi ya Senegal unaofuata jumanne hii.

“Mashabiki wetu wanapaswa kuwa makini wasijiweke kwenye hatari, kwasababu lengo la mpira ni kuleta furaha na sio kuziacha familia zikiwa na huzuni”, Amadou Makadji, meneja habari wa Feguifoot.

 

“Hatuhitaji vifo vitawale, kwahiyo tunawataka wote washangilie lakini wawe makini ili kisiwakute kitu chochote, Guinea ni nchi ambayo watu wake wanapenda sana mpira”, aliongeza Amadou.

 

Kama Guinea wataongoza kundi lao watasalia katika mji wa Yamoussoukro kwaajili ya michezo ya hatua inayofuata.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet