MASHABIKI WAFUNGUKA: "Fernandes hatufai tena kuwa nahodha Man United"
Eric Buyanza
October 16, 2026
Share :

Kiungo na nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, amekuwa nahodha wa kwanza katika historia ya klabu hiyo kupoteza mechi nyingi zaidi kuliko alizoshinda kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Takwimu hizi mbaya zimekuja baada ya United kukubali kipigo kingine cha mabao 2-0 dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumanne.
Chini ya unahodha wa Fernandes kwenye michuano hii mikubwa, United imepoteza mechi 10 na kushinda mechi 8 tu.
Mfululizo huu wa matokeo mabaya, ukihusisha na ule wa msimu uliopita ambapo United ilimaliza mkiani mwa kundi lake, umeleta mjadala mzito miongoni mwa mashabiki, huku wengi wakihoji uwezo wa uongozi wa kiungo huyo mreno.





