Mashabiki wamtaka Eriksen astaafu soka.
Joyce Shedrack
June 8, 2026
Share :
Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen anaendelea vizuri baada ya kuanguka ghafla wakati wa mechi ya kirafiki ya Denmark dhidi ya Ukraine na kukimbizwa hospitalini, huku mechi hiyo ikiahirishwa.

Baada ya tukio hilo mashabiki wengi wa soka wametoa maoni yao wakimtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kustaafu kucheza soka na kuzingatia afya yake.
Ikumbukwe, siku ya jana ni mara ya pili Eriksen kuanguka uwanjani aliwahi pia kuanguka wakati wa Mashindano ya Ulaya (Euro) mwaka 2021 dhidi ya Finland baada ya kupata mshtuko wa moyo uliosababisha moyo wake kusimama kufanya kazi kwa muda.
Kipindi hiko alipandikizwa kifaa maalumu cha kusaidia kurejesha mpigo wa moyo kinachojulikana kama Implantable Cardioverter-Defibrillator (ICD), ambacho hufuatilia na kurekebisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.





