pmbet

Mashabiki wasusia mechi ya Messi FIFA CWC

Sisti Herman

June 13, 2025
Share :

 

Baada ya muitikio mdogo wa mashabiki kununua tiketi za mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia la klabu kati ya wenyeji Inter Miami dhidi ya Al Ahly, shirikisho la soka duniani (FIFA) wameshusha bei na kuanza kugawa tiketi bure.

Kwa mchezo wa ufunguzi utaoshirikisha Inter Miami ya Lionel Messi na Al Ahly, FIFA iliungana na Chuo cha Miami Dade ili kuwapa wanafunzi tiketi moja kwa $20 na upate hadi tiketi nne za ziada bila malipo, ukitumia $4 tu kwa kila tiketi.

Pia kuna ripoti kwamba FIFA imepunguza bei katika michuano yote, huku baadhi ya tiketi zikishuka kutoka $320 hadi $52. Zinapouzwa tena, zingine zitauzwa kwa bei ndogo kama $23 na bado zinatatizika kuuza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet