pmbet

Mashahidi kuhojiwa mchakato wa Nyerere kutangazwa kuwa Mtakatifu

Sisti Herman

August 13, 2026
Share :

 

Mchakato wa kumtangaza kuwa mtakatifu Mtumishi wa Mungu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania aliyefariki mwaka 1999, umezidi kusonga mbele na sasa upo katika hatua ya kuwahoji watu (mashuhuda). Hatua hii ni muhimu sana ili kuthibitisha sifa yake ya utakatifu na maisha mazuri aliyoishi.

Askofu Msaidizi Henry Mchamungu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ambaye ni mjumbe maalum wa kusimamia mchakato huu, aliiambia ACI Africa, shirika la habari la EWTN barani Afrika, kuwa uchunguzi huo wa kikanisa unaendelea kwa kukusanya maelezo kuhusu maisha, imani, na matendo mema ya Nyerere.

"Tupo katika hatua ya kuwahoji watu, Hii ni hatua muhimu sana kwa sababu tunahitaji kuwauliza maswali ya kina ili kupata taarifa za kutosha kuhusu maisha, fadhila, na imani ya Mwalimu Nyerere."-alisema Askofu Mchamungu.

Licha ya shughuli zake za kisiasa, Nyerere alikuwa Mkatoliki mwenye msimamo thabiti wa kiroho. Alihudhuria Misa kila siku, alisali mara kwa mara, alifunga, pia alitafsiri maandiko ya Biblia kwa lugha ya Kiswahili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet