pmbet

Mashambulizi ya Iran yawasha moto ndani ya Israel

Eric Buyanza

June 14, 2025
Share :

Iran imefanya mashambulizi makubwa ya kulipa kisasi dhidi ya Israel alfajiri ya leo, hospitali moja mjini Tel Aviv iliwatibu watu saba walioumia kwenye shambulio la pili kutoka Iran, ambapo mwanamke mmoja alifariki. Saa chache baadaye, kombora la Iran lilipiga karibu na makazi ya watu katika mji wa Rishon Lezion, na kuua watu wawili na kujeruhi 19.

Katika mji wa Tehran, milio ya milipuko na makombora ya ulinzi wa anga vilisikika usiku wa manane. Uwanja wa ndege wa Mehrabad ulishika moto, huku picha zikionyesha moshi na moto mkubwa ukitanda angani.

Idara za uokoaji za Israel ziliripoti kuwa watu 34 walijeruhiwa katika eneo la Tel Aviv, na baadhi wakiokolewa kutoka kwenye vifusi. Katika eneo la Ramat Gan, magari yaliteketea na nyumba kadhaa kuharibiwa vibaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet