Mashambulizi ya Urusi yamlazimisha Zelensky kuomba msaada
Eric Buyanza
August 21, 2026
Share :

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa tena wito kwa washirika wa nchi yake kuipatia makombora kwa ajili ya mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot, kufuatia mashambulizi makubwa ya anga ya Urusi yaliyosababisha vifo vya watu 16 na kuwajeruhi karibu watu 50 katika mji mkuu Kyiv na viunga vyake.
Amesisitiza kwamba Ukraine iko tayari kununua makombora hayo badala ya kutegemea kupewa kama msaada kutoka kwa washirika wake.
Urusi imefanya tena mashambulizi makubwa usiku wa kuamkia leo, ikiulenga Kyiv na maeneo yanayouzunguka mji mkuu huo.
Kwa mujibu wa Zelensky, zaidi ya maeneo 200 yaliharibiwa, yakiwemo majengo 86.
Ameeleza kuwa Urusi ilitumia idadi kubwa ya makombora ya masafa marefu, makombora yanayoongozwa na droni katika mashambulizi hayo.
Zelensky amebainisha kuwa kiwango cha kuyadungua makombora ya masafa marefu kilikuwa chini kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na makombora yanayoongozwa.





