Mashindano ya mbio za kubeba mke Finland yageuka gumzo Duniani.
Joyce Shedrack
November 17, 2025
Share :
Kila mwaka nchini Finland, wanandoa hukusanyika kushiriki katika mashindano ya kipekee ya “Wife Carrying World Championship”, ambapo wanaume hukimbia wakipita kwenye vikwazo mbalimbali huku wakiwa wamewabeba wake zao mgongoni.

Mashindano hayo, ambayo yalianza kama utani miaka ya nyuma, sasa yamegeuka kuwa moja ya matukio makubwa yanayotambulika kimataifa na huvutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Wanandoa hushindana kwa kasi, na ushirikiano, ikiwa ni njia ya kuimarisha mahusiano na kuonyesha umoja wao.
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo hupewa zawadi ya pipa moja la bia, ikiwa ni zawadi maarufu inayotolewa kila mwaka.
Je wewe na mpenzi wako mngetoboa?





