Mashindano ya Olimpiki kumrejesha Celine Dion.
Joyce Shedrack
July 11, 2024
Share :
Mkongwe wa sanaa ya muziki kutoka nchini Canada Celine Dion huwenda akatumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki inayofanyika jijini Paris,Ufaransa 2024.
Msanii huyo ambaye hivi karibuni alifunguka namna ambavyo alificha ugonjwa unaomsumbua licha ya kuwa dalili zake alianza kuziona mwaka 2008 ugonjwa huo unaosababisha mwili wake kudhoofika unatambulika kama Stiff Person Syndrome (SPS) unaokena kutokuwa kikwazo kwake kukamilisha show yake.
Mashindano hayo ya Olimpiki yanatarajia kuanza Ijumaa, Julai 26 mwaka huu na kumalizika Agosti 11, 2024, jijini Paris nchini Ufaransa.
Wasanii wengine wanaotarajia kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo ni pamoja na Dua Lipa kutoka Albanian na Aya Nakamura kutokea Paris.