pmbet

Mashine ya mabao yarejea Msimbazi

Sisti Herman

January 11, 2024
Share :

Simba Queens wamethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji wao zamani Jentrix Shikangwa ambaye alitimkia barani Asia mwishoni mwa msimu jana kucheza soka la kulipwa kunako klabu ya Beijing Professional FC ya ligi kuu soka nchini China.

 

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Kenya amerejea Msimabazi baada ya dili lake ya muda mfupi wa miezi 6 kufikia ukomo nchini China kwenye kwenye dirisha hili.

 

Ikumbukwe Jentrix aliondoka baada ya kufunga mabao 17 kwenye mechi 16 za ligi kuu wanawake Tanzania akiwa na Simba ambayo alijiunga nayo mwanzoni mwa msimu akitoka kucheza soka barani Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet