Mashine za mabao zapishana mlangoni Simba
Sisti Herman
January 23, 2024
Share :
Dirisha hili la usajili kwa upande wa Simba limeshihudia kuachwa kwa kinara wa mabao kwenye timu yao msimu huu Jean Baleke ambaye anaondoka kaiwa na mabao 8 kwenye ligi kuu Tanzania bara pamoja na Mshambuliaji wao raia wa Zambia Moses Phiri ambao waliongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Lakini wekundu hao wa msimbazi wameingiza mashine ya mabao ambayo inaongoza kwenye msimamo wa wafungaji kwenye ligi kuu Zambia, Michael Fred raia wa Ivory Coast ambaye mpaka anasajiliwa Simba tayari alishatupia kimiani mabao 14 kwenye mechi 18 msimu huu.
Je Michael Fred ataweza kuziba pengo la Baleke? hili ni swali linalopitapita kwenye vichwa vya mashabiki wa Simba, tusubiri tuone, wana Simba wanamdai.