Mashujaa Srengeti boys watua Dar wakitokea Morocco.
Joyce Shedrack
June 3, 2026
Share :
Vijana wa timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania U17 - Serengeti Boys wamewasili Jijini Dar es Salaam wakitokea Rabat Morocco, ambako jana walicheza fainali ya AFCON U17 na SENEGAL na kupoteza kwa penati 4-2 baada ya sare ya 1-1 90’.
Serengeti boys wamewasili kishujaa wakiwa na tuzo zote za michuano hiyo sipokuwa tuzo ya golikipa bora wa mashindano iliyochukuliwa na Senegal huku wakipokelewa na mamia ya watu walijitokeza uwanja wa ndege.





