pmbet

Mashujaa vs Simba"Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi"Julio.

Joyce Shedrack

May 13, 2026
Share :

Kocha Mkuu wa Mashujaa Jamhuri Kihwelu Julio amezungumza kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

 

Julio amekiri kuwa anaiheshimu klabu ya Simba kwa kuwa ni timu kubwa yenye uwekezaji lakini Mashujaa pia ni timu kubwa na ukubwa wa pua si wingi wa makamasii.

 

"Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi, mimi Simba SC nilikuwepo kama mchezaji nikaja nikawa kocha na saivi Kocha ni Matola na Mzungu hata jina simjui, Siwafahamu uchezaji wao na siwaogopi ila ni timu kubwa kwenye uwekezaji lakini Mashujaa FC ni timu kubwa vilevile."Amesema kocha Julio.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet