Mashujaa yamrejesha Samson Madeleke.
Joyce Shedrack
August 13, 2025
Share :
Klabu ya Mashujaa Fc imemrejesha beki wake wa kati Samson Madeleke mwenye umri wa miaka 24 raia wa Tanzania akitokea Pamba Jiji Fc.
Madeleke ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Mbeya City anarejea Mashujaa baada ya msimu uliopita kukiwasha na Pamba Jiji.