Massawe ajitosa ubunge Moshi vijijini
Sisti Herman
July 3, 2025
Share :
Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara na watoa huduma Tanzania, Bw. Martin Massawe, amechukua fomu kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi, kugombea ubunge Jimbo la Moshi vijijini.
Massawe ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro, amechukua fomu hiyo leo Julai 2, 2025 ambapo amekabidhiwa na katibu wa chama hicho Wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhan Mahanyu.