Mastaa wa Mamelodi waliokuwa Nationa Team waiwahi Yanga
Sisti Herman
March 28, 2024
Share :
Mastaa wa Mamelodi Sundwons waliokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Afrika kusini iliyokuwa nchini Algeria kushiriki FIFA Series 2024 wamewasili jijini Dar es Salaam Alfajiri ya leo kwaajili ya kujiunga na kambi ya klabu yao inayojiandaa kucheza mchezo wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Yanga mchezo utakaochezwa uwanja wa Mkapa.
Mastaa hao ni pamoja na kipa na nahodha wa Afrika kusini Ronwen Williams, Teboho Mokoena, Aubrey Modiba, Thapelo Morena, Grant Kekana na Themba Zwane ambaye inatajwa kuwa kikanuni hatocheza mchezo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.