pmbet

Mastaa wahudhuria msiba wa Zuchy

Sisti Herman

April 29, 2024
Share :

Wasanii mbalimbali wamejitokeza kwenye viwanja vya Leaders Club leo Aprili 29, 2024 kumuaga marehemu Noel Mwingila (Zuchy) aliyekuwa mpiga picha na mwandishi wa habari wa Millardayo na Ayo Tv na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Mastaa hao ni Hamisa Mobeto, Shamsa Ford na mume wake, Hussein Lugendo (Mlilo), Shilole na Zaiylissa akiwa na mume wake Haji Manara wakiwa miongoni mwa waombolezaji waliofika kwenye viwanja hivyo.

Zuchy alifariki dunia alfajiri ya Ijumaa Aprili 26, 2024, eneo la Makonde, mkoani Dar es Salaam katika ajali ya bodaboda. Katika ajali hiyo, dereva bodaboda ambaye jina bado halijafahamika alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet