Mataifa masikini yakabiliwa na wimbi madeni ya China
Eric Buyanza
May 27, 2025
Share :
Ripoti iliyochapishwa na shirika la kimataifa nchini Australia imetaja hali ngumu ya kiuchumi inayoyakabili mataifa masikini duniani kutokana na mzigo wa madeni ya China, ambayo mwaka huu wa 2025 yamevunja rikodi.
Taasisi ya Lowly inayofuatilia kiwango cha madeni ulimwenguni imesema mradi wa miundombinu wa China, maarufu kama BRI, uliotowa mikopo mikubwa kwa ajli ya ujezi wa bandari, reli, barabara na majengo katika mataifa ya Afrika, Asia na Pasifiki, umesababisha kiwango kikubwa cha madeni kwa mataifa hayo yanayoendelea.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ndani ya muongo huu, China itakuwa mnufaika mkubwa wa kukusanya madeni yake badala ya kuwa muwekezaji kwenye mataifa hayo, huku nchi zilizokopeshwa zikiingia kwenye wimbi kubwa la ufukara kutokana na kulipa madeni hayo.
DW