pmbet

Mate kutumika kupima Sukari badala ya Damu

Sisti Herman

April 15, 2024
Share :

Naibu Waziri wa wizara ya Afya Mh. Godwin Mollel amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza kwenye teknolojia kwenye huduma mbalimbali za afya ambapo kwa kuanzia sasa wagonjwa wa Kisukari kwenye hospitali ya Muhimbili wataanza kupimwa mate kujua kiwango cha sukari badala ya kutolewa damu.

“Rais wetu [Samia Suluhu] alikwenda Marekani akakutana na Chuo Kikuu cha Carolina, imefanya revolution [mapinduzi] kubwa sana, tunaanza kesho kutwa Muhimbili, wagonjwa wote wa kisukari hawatatobolewa tobolewa tena. Inakuja teknolojia kwa kushirikiana na South Carolina na sasa mtaanza kupimwa, mnachukua tu mate mnaangalia sukari bila kuhitaji kujitoboa kila siku.” - Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

Cc; Swahili times

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet