Matonya apandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubakaji Kenya.
Joyce Shedrack
April 10, 2026
Share :
Msanii wa Bongo Fleva, Sefu Shabani maarufu kama Matonya amefikishwa mahakamani nchini Kenya akikabiliwa na shtaka la ubakaji.
Kwa mujibu wa Daily Nation, anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2026 huko Nyali, Mombasa, kwa kumuingilia kimwili mwanamke bila ridhaa yake. Pia anakabiliwa na shtaka mbadala la kumgusa isivyo halali.
Mahakama imempa dhamana ya Sh500,000 za Kenya sawa na milioni 10 za Tanzania akiwa na mdhamini mmoja.
Mfanyabiashara maarufu Cheifgodlove amejitolea kumuwekea dhamana ili atoke.





