pmbet

Mavazi ya Bianca, ni ubunifu wa Dada yangu, Kanye West hausiki - Angelina Censori

Eric Buyanza

April 1, 2024
Share :

Rapa Kanye West amekuwa akikosolewa vikali sehemu mbalimbali duniani kwa namna ambavyo mke wake Bianca Censori amekuwa akivaa huku baadhi ya magazeti ya ulaya yakisema Baba yake Bianca anamchukia sana Kanye kutokana na uvaaji wa binti yake.
 

Bianca mara zote amekuwa akivaa mavazi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake.
 

Kwa mujibu wa dada wa Bianca, aitwae Angelina Censori, amesema mtindo huo wa mavazi ni ubunifu wa dada yake.
 

Katika mahojiano na gazeti la 'Herald Sun' la nchini Australia, Angelina amedai kuwa taarifa zozote za kwamba baba yao anachukizwa na jinsi Kanye anavyoishi na mtoto wake, sio za kweli kwani baba yao anaiunga mkono kwa asilimia 100 ndoa ya wawili hao.
 

Hivi ndivyo Angelina Censori alisema:
 

"Sote tunamuunga mkono Kanye. Tunaunga mkono albamu yake mpya. Tunaunga mkono nguo zake mpya anazoachia. Kulikuwa na kitu kinasemwa kuhusu baba yangu hivi karibuni. Baba yangu huwa haongeagi kamwe. Hakuna ukweli wowote."
 

Ripoti iliyotolewa na gazeti la Daily Mail hivi karibuni ilidai kuwa Baba wa Bianca huwa hafurahishwi na jinsi binti yake anavyovaa akiwa hadharani na anamchukia sana Kanye kwasababu hiyo.  
 

Hapo awali, kulikuwa na chuki nyingi zilizoelekezwa kwa Kanye West kutokana na mavazi ya mkewe, wengi wakidhani yeye ndiye anayemshawishi uvaaji huo... lakini kauli hii ya shemeji yake imemuweka Kanye West huru.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet