Mawakili 30 wako mahakamani kumtetea Lissu leo
Eric Buyanza
June 2, 2025
Share :
Jumla ya mawakili 30 akiwemo Wakili Peter Kibatala na Dk Rugemeleza Nshala wapo mahakamani kumtetea mwanasiasa na wakili wa kujitegemea Tundu Antiphas Lissu katika kesi zake mbili za jinai zitakazosikilizwa leo Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Kesi hizo ambazo zinasikilizwa hadharani, zinarushwa mubashara kwa umma kupitia mitandao rasmi ya Mahakama ya Tanzania na Chaneli zingine mbalimbali.