Mayele afunga tena, Pyramids wakishinda ugenini
Sisti Herman
April 16, 2024
Share :
Urafiki wa mshambualiaji Fiston Mayele na nyavu haujawahi kuisha, licha ya wiki iliyopita kuzua gumzo na kutikisa vyombo mbalimbali vya habari nchini kutokana na mahojiano aliyofanya na Azam Tv, nyota huyo haonekani akitoka mchezoni na mambo ya nje ya uwanja baada ya jana kufunga goli moja akiwa na timu ya yake Pyramids.
Mayele alifunga goli moja kwenye ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Al Mokawloon kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Misri na kuisaidia timu yake kuzoa alama zote tatu.
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Yanga hadi sasa kwenye ligi kuu nchini humo amecheza mechi 14 na kufunga magoli 5 huku akitoa pasi za mabao 2.