Mayele akitaka kiatu cha dhahabu kimyakimya Misri
Sisti Herman
June 24, 2024
Share :
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga Fiston Mayele ameendelea kuonyesha uwezo wake mkubwa wa 'kucheka na nyavu' baada ya jana kufunga mabao mawili na kusaidia klabu yake mpya ya Pyramids kushinda 3-1 dhidi ya Al Mokawloon kwenye mchezo wa ligi kuu Misri.
Mabao hayo mawili yamemfanya Mayele kufikisha mabao 11 kwenye ligi hiyo na kuwa wa pili kwenye orodha kwenye Orodha ya wanaoongoza kwa kufunga mabo mengi kwenye ligi hiyo inayoongozwa na Hossam Ashraf wa Baladiyet El Mahallah mwenye mabao 12.
Hizi ni takwimu za Mayele kwenye ligi kuu nchini Misri msimu huu;
- Mechi 24
- Magoli 11
- Asisti 3
Je Mayele ataweza kutwaa kiatu cha ufungaji bora?