Mayele aongoza mastaa wanaoendesha droo ya AFCON U17
Sisti Herman
April 8, 2026
Share :

Wachezaji maarufu wa ligi kuu Misri Fiston Mayele wa Pyramids, Aliou Dieng wa Al Ahly na Ahmed Belhadj wa Ceramica Cleopatra FC wamechaguliwa kuendesha droo ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika chini ya miaka 17.

Kwenye droo hiyo leo timu ya Taifa ya Tanzania (Serengeti Boys) wapo poti namba 3 kati ya mapoti manne yenye timu 4 kila mmoja.





