pmbet

Mayele kurudi Tanzania,Yanga kuanzia Burundi,Azam kukipiga na APR.

Joyce Shedrack

July 11, 2024
Share :

Droo ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika imekamilika wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo wakijua wapinzani watakaokutana nao katika hatua ya awali.

Mabingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara Yanga watakutana na Vital'o fc ya Burundi huku Yanga akianzia ugenini.

Matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam fc watakutana na APR ya Nchini Rwanda.

Timu zote hizo zikishinda michezo hiyo ya hatua ya awali watacheza raundi ya kwanza ya michuano hiyo ili kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza hatua ya makundi.

Mshindi wa Vital'O v Young Africans SC. Atakutana na Mshindi kati ya SC Villa (Uganda) v Commercial Bank (Ethiopia)

Mshindi wa AZAM FC V APR Atakutana na Mshindi wa JKU (Zanzibar) v Pyramid (Misri).

Huwenda tukamshuhudia Fiston Kalala Mayele aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga akirejea Tanzania kucheza dhidi ya Azam endapo Azam fc atafanikiwa kumwondosha APR na Pyramid akimtoa JKU ya Zanzibar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet