Mayele na Aziz Ki uso kwa uso
Sisti Herman
January 11, 2024
Share :
Wachezaji waliowahi kucheza wote pamoja wakiwa na wananchi Yanga Sc, Fiston Mayele ambaye alitimkia Pyramid ya Misri na Stefanie Aziz Ki wamekutana tena kwenye mchezo wa kirafiki uliowakutanisha timu zao za Taifa Congo DR na Burkina faso zinazojiandaa na michuano ya AFCON inayotegemewa kuanza wikiendi hii nchini Ivory Coast.
Burkinafaso ya Aziz Ki iliiadhibu Congo ya Mayele mabao 2-1 hku mabao ya Burkinabe yakifungwa na washambuliaji Ibrahim Toute na Mohamed Konate huku bao pekee la Congo likifungwa na Chancel Mbemba.
Kwenye AFCON, Congo ipo kundi F na timu za Tanzania, Zambia na Morocco huku Burkinabe wakiwa kundi D na timu za Algeria, Angola na Mauritania.