pmbet

Mayweather kurejea ulingoni baada ya pambano na Tyson

Eric Buyanza

February 21, 2026
Share :

Floyd Mayweather Jr. anatarajiwa kurejea kwenye mapambano ya kulipwa baada ya miaka 9 tangu apigane na Conor McGregor mwaka 2017.
 

Mbabe huyo anayeshikilia rekodi ya kutopigwa anatarajiwa kuzichapa na bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Mike Tyson, ambaye ana miaka 59, kwenye pambano litakalofanyika mwezi Aprili 2026, kabla ya kurejea kwenye mapambano ya kulipwa baadaye mwaka huu.
 

Mayweather, ambaye ana miaka 48 anataka kuonyesha kwamba bado ana uwezo wa kuweka rekodi mpya kwenye ulingo.
 

Pambano la Mayweather na Tyson linatarajiwa kufanyika tarehe 25 Aprili 2026, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Muhammad Ali na George Foreman walipigana mwaka 1974.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet