Mayweather kurudiana na Pacquiao tena mwaka huu
Sisti Herman
February 24, 2026
Share :

Manguli wa ndondi Floyd Mayweather Jr. na Manny Pacquiao wamethibitisha rasmi pambano la marudiano linalosubiriwa kwa hamu tarehe Septemba 19, 2026.
Pambano hili la kihistoria litafanyika katika ukumbi wa kisasa wa Sphere jijini Las Vegas, ikiwa ni zaidi ya miaka 11 tangu walipokutana kwa mara ya kwanza.
Katika mabadiliko makubwa ya kimichezo, pambano hilo litarushwa mubashara duniani kote kupitia mtandao wa Netflix.





