Mazungumzo ya Israel na Hamas yakamilika bila ya maazimio
Eric Buyanza
July 7, 2025
Share :
Awamu ya kwanza ya mazungumzo kati ya Israel na Kundi la Hamas, yamemalizika nchini Qatar, bila ya wajumbe kutoka na maazimio ya uhakika kuhusu makubaliano ya kusitisha vita ya Gaza, vyanzo mbalimbali vimethibitisha.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, ujumbe wa Israel uliotumwa Doha, haukuwa na mamlaka ya kuamua makubaliano yoyote na Hamas, tofauti na kauli ya serikali ya israel ambayo ilisema ilituma maofisa wa juu katika serikali.
Mazungumzo haya yamefanyika saa chache kabla ya Waziri mkuu Benjamin Netanyahu, hajapanda ndege kuelekea Washington ambako atakutana kwa mazungumzo na Rais Donald Trump.
Awali kuelekea mazungumzo ya Doha, rais Trump, alisema kuna uwezekano mkubwa wa kufikia makubaliano na Hamas kuhusu kuachiliwa kwa mateka inaoendelea kuwashikilia walio hai na waliokufa.