Mbabe wa Assad akutana na Putin ikulu ya Moscow
Eric Buyanza
October 16, 2025
Share :
Rais Vlamidir Putin wa Urusi amekutana na kiongozi mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa mjini Moscow.
Putin ametumia mazungumzo yao kuusifu uhusiano kati ya nchi hizo mbili hata baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar al-Assad aliyekuwa mshirika mkubwa wa Urusi.
Hiyo ilikuwa ziara ya kwanza ya Al-Sharaa nchini Urusi tangu alipochukua hatamu za uongozi nchini Syria kwa kuongoza uasi ulioungusha utawala wa Assad, Disemba mwaka jana. Assad alikimbilia Urusi na kuomba hifadhi ya kisiasa.
Viongozi hao wawili walizungumzia hatma ya kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria pamoja na ushirikiano kwenye sekta za uchumi na maendeleo hususani nishati, uchukuzi na utalii.
Putin amesema Syria inapitia kipindi kigumu lakini uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni umeimarisha ushirikiano baina ya makundi ya kisiasa.