Mbabe wa vita aliyewahi kula moyo wa binadamu, jela miaka 30
Eric Buyanza
March 29, 2024
Share :
Mahakama nchini Ufaransa jana imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa mbabe wa kivita nchini Liberia, Kunti Kamara, baada ya kumkuta na hatia ya makosa ya unyanyasaji dhidi ya raia na kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kamara, mwenye umri wa miaka 49 hivi sasa, awali alikuwa amehukumiwa kifo wakati kesi yake iliposikilizwa kwa mara ya kwanza jijini Paris mwaka wa 2022.
Katika ushahidi uliowashtua wengi, Kamara anadaiwa kula moyo wa mwalimu mmoja wakati wa vita hivyo ambapo ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulitendeka.
Aidha amepatikana na kosa la kukiuka haki za binadamu kwa kushindwa kuwazuia wapiganaji waliokuwa chini yake kuwabaka wasichana wenye umri mdogo mwaka 1994.
Watu zaidi ya laki mbili waliuawa wakati wa machafuko yaliotokea katika taifa hilo la Afrika Magharibi kati ya mwaka wa 1989 na 2003.