Mbakaji aangua kilio baada ya kuambiwa aliyembaka ameathirika
Eric Buyanza
April 29, 2024
Share :
September mwaka 2013, Mahakama ya mjini Liverpool nchini Uingereza ilimhukumu Richard Thomas kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kubaka.
Richard Thomas, aliyekuwa na miaka 27 wakati huo, alianguka chini ndani ya mahakama wakati polisi walipomjulisha kuhusu hali ya kiafya ya mwanamke aliyembaka.
Picha hapo inamuonesha Thomas akilia kwa uchungu, hata hivyo kilio hicho sio kwasababu ya hukumu, bali ni baada ya kuambiwa kuwa mwanamke aliyembaka ni mwathirika wa virusi vya ukimwi.