Mbappe afungua akaunti ya mabao La Liga
Sisti Herman
September 2, 2024
Share :
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappé jana usiku amefungua akaunti yake ya magoli akiwa na klabu ya Real Madrid kwenye Ligi Kuu ya Uhispania baada ya kufunga magoli mawili na kuwaongoza mabingwa hao watetezi wa Laliga kushinda 2-0 dhidi ya Real Betis katika dimba la Santiago Bernabéu jijini Madrid.
Mbappé alifunga goli lake la kwanza dakika ya 67 kwa pasi safi ya kisigino ya Ferderico Velverde huku akiongoeza lingine dakika ya 75 kwa mkwaju wa penati.
Kwa ushindi huo Real Madrid imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza (unbeaten) kufikia mechi 35 kwenye Laliga.