pmbet

Mbappe akiri yeye ni mshambuliaji namba 4 Real Madrid.

Joyce Shedrack

May 15, 2026
Share :

Kylian Mbappe anadai kuwa ameambiwa yeye ni 'mshambulizi chaguo la nne' katika klabu ya Real Madrid baada ya kuanzia benchi dhidi ya Real Oviedo, lakini maneno ya Mfaransa huyo yalikanushwa haraka na kocha Alvaro Arbeloa.

 

Mbappe alianzia benchi baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha, lakini aliingizwa dakika ya 69 akichukua nafasi ya Gonzalo Garcia, ambaye aliipatia Real Madrid bao la kuongoza kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 2-0.

Kylian Mbappe jeered on Real Madrid return - BBC Sport

Mfaransa huyo baada ya kuingia alipokewa na kelele za kuzomewa kutoka kwa mashabiki wa uwanja wa Bernabeu, amesema anakabiliwa na changamoto lakini atazifanyia kazi na anamheshimu kocha kwa kiła analoamua kwa aijli ya manufaa ya timu.

 

"Niko sawa kwa asilimia 100," Mbappe aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

 

'Sikucheza kwa sababu kocha aliniambia mimi ni mshambuliaji wa nne kwenye kikosi nyuma ya (Franco) Mastantuono, Vini (Vinícius Júnior) na Gonzalo (García). 
 

'Ninaikubali na kucheza wakati niliopewa. Nadhani nilicheza vizuri. 'Nilikuwa tayari kuanza. Sina hasira na kocha, lazima kila wakati uheshimu uamuzi wa kocha.

 

'Nitajitahidi kurejea kwenye kikosi cha kwanza.’

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet