Mbappe aonyesha heshima kubwa kwa Modric
Sisti Herman
March 20, 2025
Share :
Nyota wa Real Madrid Kylian Mbappe ameonyesha kuwa na heshima kubwa na nyota mwenzake wa klabu hiyo Luka Modric ambaye leo watakutana wakiwa wapinzani na timu zao za Taifa, Ufaransa ya Mbappe na Croatia ya Modric.
"Namheshimu sana Modric, tangu wakati nakuwa namuona akicheza na hadi sasa yupo kwenye ubora wake lakini pia ni nahodha wetu Madrid kwahiyo nategemea kujifunza zaidi kwake" alisema Madrid akiongea na vyombo vya habari.
Mbappe ameyasema hayo baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari kuhusu picha aliyopiga akiwa mtoto huku Modric akiwa mchezaji wa Madrid.
Ufaransa na Croatia watacheza leo usiku mchezo wa UEFA National League, Croatia wakiwa nyumbani.