Mbappe atambulishwa rasmi mbele ya mashabiki 85,000 Santiago Bernabeu
Sisti Herman
July 16, 2024
Share :
Ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu wathibitishe kufikia makubaliano ya kujiunga nao, Klabu ya Real Madrid leo imemtambulisha rasmi mshambuliaji na nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe mbele ya mashabiki 85,000 waliohudhuria utambulisho huo kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Mbappe ambaye pia mfungaji bora na nahodha wa PSG kwenye msimu uliomalizika utambulisho wake umeshuhudiwa pia na mchezaji bora wa zamani wa Real Madrid na Ufaransa Zinedine Zidane pamoja na magwiji wengine wa klabu hiyo.