pmbet

Mbappe atangaza kuondoka PSG, Madrid yatajwa

Sisti Herman

May 10, 2024
Share :

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na mfungaji bora wa muda wote wa PSG Kylian Mbappe ametangaza kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ikiwa zimepita siku chache toka watolewe katika nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Mbappe ambaye anahusishwa kwenda kujiunga na Real Madrid ya Hispania ametangaza kuwa anaenda kucheza soka nje ya Taifa la Ufaransa lakini hajataja Timu anayokwenda wala Nchi kitu ambacho kinaunganisha nukta kuwa safari ya kujiunga na Real Madrid imeiva.

“Leo natangaza kwamba huu ndio mwaka (msimu) wangu wa mwisho PSG sitaongeza Mkataba na safari yangu PSG nitahitimisha wiki chache zijazo, nitacheza mechi yangu ya mwisho Jumapili katika uwanja wa Parc des Princes”

“Tumekuwa pamoja kwa muda mrefu na kupata nafasi na heshima kubwa ya kuwa sehemu historia ya PSG ambayo ni Club kubwa Ufaransa “

Mbappe ametoa taarifa hiyo kupitia video maalum aliyoiandaa na kuichapisha katika ukurasa wake wa instagram na sasa mashabiki wa PSG watamuona Jumapili hii akiichezea timu yao dhidi ya Tolouse kwa mara ya mwisho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet