Mbappé avunja rekodi ya Messi, Madrid ikipiga bonge la 'Comeback'
Eric Buyanza
October 15, 2026
Share :
Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappé, ameweka historia mpya kwenye michuano ya UEFA Champions League kwa kuwa mchezaji mdogo zaidi kufikisha michezo 100 katika mashindano hayo makubwa zaidi barani Ulaya.
Mbappé amefikia hatua hiyo jana usiku, Jumatano, Oktoba 14, 2026, akiwa na umri wa miaka 27 na siku 298. Kwa kufanya hivyo, amevunja rekodi ya awali iliyokuwa inashikiliwa na nguli Lionel Messi, aliyefikisha michezo 100 akiwa na umri wa miaka 28 na siku 84. Cha kusisimua ni kwamba wachezaji wote wawili wameweka rekodi hii katika uwanja uleule wa Stadio Olimpico dhidi ya AS Roma.
Mbali na kucheza mchezo wake wa 100, Mbappé alisherehekea usiku huo kwa kufunga bao la kusawazisha katika kipindi cha kwanza.






