pmbet

Mbappe avunjika pua, kama atacheza huenda akavaa barakoa maalum

Eric Buyanza

June 18, 2024
Share :

Nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe alivunjika pua dakika za mwisho wakati timu yake ikipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Austria kwenye michuano ya Euro 2024.

Mchezaji huyo alipata jeraha hilo alipogongana na mlinzi wa Austria, Kevin Danso wakati akigombea mpira wa kichwa.

Ufaransa itamenyana na Uholanzi siku ya Ijumaa na kuna mashaka kama mchezaji huyo atacheza.

Hata hivyo tathmini za kiafya zinafayika kuona kama ataweza kuvalishwa barakoa maalum ili aweze kucheza mchezo huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet