Mbappe aweka rekodi ya mechi 100 UCL
Sisti Herman
October 16, 2026
Share :

Nyota wa Real Madrid Kylian Mbappé, kwa mara nyingine ameandika historia katika Ligi ya Mabingwa kwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia kufikisha mechi 100 katika Ligi ya Mabingwa, huku akiwa amefunga mabao 7️⃣2️⃣… hadi sasa.
Akiwa na umri wa miaka 27 na siku 298 pekee, Kylian anavunja rekodi ya Lionel Messi iliyokuwa ya miaka 28 na siku 84… na hivyo kujiunga na kundi la wasomi.
Mbappé amempiku Raúl na kuingia katika orodha ya wafungaji 5️⃣ 𝐁𝐎𝐑𝐀 𝐙𝐀𝐈𝐃𝐈 katika historia ya Ligi ya Mabingwa (UCL):
1️⃣ Cristiano Ronaldo — mabao 140
2️⃣ Lionel Messi — mabao 129
3️⃣ Robert Lewandowski — mabao 107
4️⃣ Karim Benzema — mabao 90
🆕5️⃣ Kylian Mbappé — mabao 72





