pmbet

Mbappe, Dembele wampa magoli yao Jota

Sisti Herman

July 6, 2025
Share :

 

Nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe na Osmane Dembele kwa nyakati tofauti leo wameonyesha ishara za kutoa heshima kwa mchezaji wa Liverpool na Ureno Diogo Jota aliyefariki kwa ajali ya gari. 

 

Dembele alitoa heshima yake kwa jota baada ya kushangilia kwa staili ya Jota ya kucheza 'playstation' kwenye mchezo wa robo fainali kati ya PSG dhidi ya Bayern Munich, PSG ikishinda 2-0. 

 

Mbappe alitoa heshima yake kwa jota baada ya kushangilia kwa staili ya kuonyesha herufi za namba ya jezi ya Jota (20) kwenye mchezo wa robo fainali kati ya Real Madrid dhidi ya Borrusia Dortmund, Madrid ikishinda 3-2. 

 

Jota alifariki mjini Zamora nchini Hispania siku ya Alhamis Julai 3 kwaajali ya gari alipokuwa akisafiri kutokea Ureno kuelekea Uingereza na kuzikwa jana Jumamosi Julai 5 huko nchini kwao Ureno.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet